Rais wa Venezuela Hugo Chavez 57 ambaye hapo mwazo alifanyiwa upasuaji ili kuondoa uvimbe wa kansa nchini Kuba, amerejea tena nchini humo kwa ajili ya kufanya upasuaji mwingine. Siha ya raisi huyo ilipelekea wataalamu wa mambo ya kisiasa nchini Venezuela kuuulizana kama rais Chavez ataweza kuongoza nchi tena ikiwa atachaguliwa katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi wa Oktoba 2012. Rais Hugo Chavez aliwatoa wasiwasi wananchi wake na kuwaambia wasiwe na shaka kuhusiana na siha yake.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 299186
ABNA inatuhabarisha kuwa:Rais wa Venezuela amewasili nchini Cuba kwa minajili ya kufanyiwa upasuaji